DOAJ Open Access 2026

Uchanganuzi wa Ubanaji wa Maana za Maneno Katika Jukwaa la “Facebook”

Simon Peter Katui

Abstrak

Makala hii inachanganua ubanaji wa maana za maneno katika jukwaa la Facebook. Suala la ubanaji wa maana za maneno katika mawasiliano limewavutia wasomi kadhaa. Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanyika kuhusu ubanaji wa maana za maneno katika jukwaa la Facebook. Makala hii imejikita katika kuchanganua ubanaji wa maana za maneno pamoja na kiini cha matumizi ya ubanaji huo katika jukwaa la Facebook. Makala hii iliongozwa na Nadharia ya Semantiki Leksika ya Blutner (1998). Mkabala wa makala hii ni wa kimaelezo. Sampuli ya utafiti huu ilikuwa ya kimakusudi, ambapo tuliteua vikundi vitatu vya mawasiliano katika jukwaa la Facebook kwa hiari. Data iliyotumika katika makala hii ilikusanywa kati ya mwezi Aprili na Oktoba mwaka wa 2020.Vikundi vya mawasiliano kwenye jukwaa la Facebook vilitumika. Data hii ilikusanywa kwa ajili ya tasnifu ya uzamili iliyoshughulikia suala la Uchanganuzi wa Kipragmatiki wa Maana ya Mawasiliano katika Jukwaa la Facebook. Tulipitia kurasa za makundi ya mawasiliano katika jukwaa la Facebook na kunakili data husika. Tulichanganua data tuliyoinakili ili kupata lengo la ubanaji wa maana za maneno kwenye jukwaa la Facebook. Data iliyokusanywa kuhusu mada hii inaonesha kwamba mawasiliano katika jukwaa la Facebook husheheni matumizi ya ubanaji wa maana za maneno.  Kwa kuzingatia Mkabala wa Pragmatiki, makala hii inaonesha kwamba watu hutumia ubanaji wa maana za maneno. Watu hubana maana za maneno kwa ajili ya kusetiri ujumbe na kuhifadhi heshima na taadhima kwa wanakikundi. Maana za maneno hubanwa kulingana na mazingira ya usemi husika kwa nia ya kuleta umoja.

Penulis (1)

S

Simon Peter Katui

Format Sitasi

Katui, S.P. (2026). Uchanganuzi wa Ubanaji wa Maana za Maneno Katika Jukwaa la “Facebook”. https://doi.org/10.58721/jkal.v4i1.1591

Akses Cepat

PDF tidak tersedia langsung

Cek di sumber asli →
Lihat di Sumber doi.org/10.58721/jkal.v4i1.1591
Informasi Jurnal
Tahun Terbit
2026
Sumber Database
DOAJ
DOI
10.58721/jkal.v4i1.1591
Akses
Open Access ✓