DOAJ Open Access 2025

Mchango wa TEHAMA na Changamoto Zake katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Msamiati wa Kiswahili Tanzania

Ernest Daimon Haonga

Abstrak

Makala hii inachunguza mchango wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na changamoto zake katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Tanzania. Shabaha kuu ilikuwa kubainisha namna TEHAMA inavyochangia katika mbinu za ufundishaji, kuongeza ufanisi wa ujifunzaji, na kuimarisha mawasiliano ya kielimu katika mazingira ya kidijitali. Makala hii ilitumia mkabala wa kimaelezo, ambapo data zilikusanywa kupitia hojaji na mahojiano. Watoataarifa waliohusika ni walimu wa Kiswahili, wanafunzi kutoka vyuo teule vya elimu ya juu, wataalamu wa lugha na wataalamu wa TEHAMA walioteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa. Makala iliongozwa na Nadharia ya Ujifunzaji wa Kielektroniki, inayosisitiza jinsi watu wanavyopokea, kuchakata na kuhifadhi maarifa kupitia vifaa vya kidijitali. Nadharia hii inaeleza kwamba ujifunzaji wa lugha unaweza kuboreshwa kupitia matumizi ya maandishi, picha, sauti, na mwingiliano wa kidijitali. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa TEHAMA imeongeza motisha ya wanafunzi, kupanua mbinu za ufundishaji, na kurahisisha upatikanaji wa rasilimali za kujifunzia msamiati wa Kiswahili. Hata hivyo, changamoto kama upungufu wa vifaa, ujuzi mdogo wa walimu, na ubovu wa miundombinu ya mtandao bado zinakwamisha ufanisi wa matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa msamiati wa lugha. Kwa jumla, makala inadhihirisha kuwa TEHAMA ni nyenzo muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili licha ya changamoto za miundombinu zilizopo.

Penulis (1)

E

Ernest Daimon Haonga

Format Sitasi

Haonga, E.D. (2025). Mchango wa TEHAMA na Changamoto Zake katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Msamiati wa Kiswahili Tanzania. https://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1430

Akses Cepat

PDF tidak tersedia langsung

Cek di sumber asli →
Lihat di Sumber doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1430
Informasi Jurnal
Tahun Terbit
2025
Sumber Database
DOAJ
DOI
10.58721/jkal.v3i2.1430
Akses
Open Access ✓