DOAJ Open Access 2024

Viashiria vya Kujiua: Uchunguzi wa Mhusika Kazimoto katika Riwaya ya Kichwamaji

Adria Fuluge

Abstrak

Wahusika katika kazi za fasihi huumbwa kwa ustadi mkubwa kwa lengo la kubeba tafakuri na fikra za mtunzi kuhusu maisha ya jamii. Katika uumbaji huo, aghalabu, binadamu husawiriwa kama kiumbe anayeteseka na anayeishi katika ulimwengu usiomjali, aliyezungukwa na mateso na ubwege[1], na anayeshindwa kukabiliana vyema na uhalisia wake (Wamitila, 2002). Mambo hayo, ndiyo huweza kusababisha afanye maamuzi fulani kama vile kujiua. Hivi ndivyo anavyofanya Euphrase Kezilahabi katika riwaya ya Kichwamaji (1974) anapomuumba mhusika anayejiua. Hata hivyo, kwa kuwa kujiua huambatana na viashiria mbalimbali, makala haya yanajadili viashiria vya kujiua kwa mhusika mkuu katika riwaya teule tu. Riwaya hiyo imeteuliwa kwa sababu ina mawanda ya kutosha yaliyowezesha kupata data zilizolengwa katika makala haya. Pia, riwaya hiyo imeteuliwa kama sampuli ya kuwakilisha riwaya nyingine zenye viashiria vya kujiua. Misingi ya Nadharia ya Udhanaishi imetumika katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini. Mjadala umebainisha kwamba katika riwaya ya Kichwamaji vipo viashiria vinne vya kujiua vilivyomkumba Kazimoto kabla ya kujiua kwake. Viashiria hivyo ni kukata tamaa, kujitenga kijamii, kuzungumzia masuala ya kujiua na mabadiliko ya tabia. Makala yanahitimisha kwamba jamii inahitaji kupewa elimu ya kutosha kuhusu kujiua kwa wahusika pamoja na viashiria vyake ili iweze kumtambua na kumsaidia mtu mwenye viashiria vya kujiua.   [1]Mtazamo wa kidhanaishi unaopinga kuwepo kwa maana na ufahamu katika maisha ya binadamu, kutokana na kukata tamaa na kukosa tumaini la kuishi. Kwa mujibu wa Esslin (2001), ubwege ni hali ya kukosa nia ya kufanya jambo fulani na kutengwa katika imani za kidini, tabia za kiungu na mizizi ya akili na mawazo ya mtu. Hii ina maana kwamba ubwege ni kitendo cha kudadisi hali ya binadamu ya kuendelea kuishi ilhali maisha hayana maana tena.

Penulis (1)

A

Adria Fuluge

Format Sitasi

Fuluge, A. (2024). Viashiria vya Kujiua: Uchunguzi wa Mhusika Kazimoto katika Riwaya ya Kichwamaji. https://doi.org/10.58721/jkal.v2i1.548

Akses Cepat

PDF tidak tersedia langsung

Cek di sumber asli →
Lihat di Sumber doi.org/10.58721/jkal.v2i1.548
Informasi Jurnal
Tahun Terbit
2024
Sumber Database
DOAJ
DOI
10.58721/jkal.v2i1.548
Akses
Open Access ✓